Job 33:8-12


8“Lakini umesema nikiwa ninakusikia,
nami nilisikia maneno yenyewe:
9 a‘Mimi ni safi na sina dhambi;
mimi ni safi na sina hatia.
10 bLakini bado Mungu amepata dosari kwangu,
naye ananiona kama adui yake.
11 cAnanifunga miguu kwa pingu,
tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’

12 d“Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa,
kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
Copyright information for SwhNEN